Nchini England mabingwa watetezi wa Ligi ya nchi Hiyo Manchester United wameendelea na mwanzo mbaya wa ligi hiyo baada ya hii leo kukubali kipigo cha bao moja bila toka kwa Newcastle United .
Bao pekee lililoacha simanzi kwa mashabiki wa United lilifungwa na kiungo Mfaransa Yohan Cabaye. Matokeo haya yanaiacha United kwenye nafasi ya tisa wakiwa wameachwa na vinara wa ligi hiyo kwa pointi 12.
Hii ni mara ya kwanza kwa United kupoteza mechi mbili mfululizo kwenye uwanja wake wa nyumbani tangu mwaka 2002 huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa Newcastle United kushinda mchezo kwenye uwanja wa Old Trafford kwa miaka 41.