Watu 11 wamepoteza maisha papo hapo na mwingine mmoja kufariki dunia akiwa njiani akipelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando,baada ya kutokea ajali mbaya ya gari iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Luhuye T 410 AWQ lililokuwa likitokea Tarime Mkoani Mara kwenda jijini Mwanza.
Basi hilo liligonga nyumba kisha kupinduka leo saa tano na dakika 10 asubuhi katika barabara ya Mwanza – Mara katika kijiji cha Yitwimila kata ya Kiloleli wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.
Mbali na watu 12 kufariki dunia pia watu 60 wamejeruhiwa ambapo imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo kasi wa sasi hilo ambapo dereva wa alishindwa kumudu gari hilo likiwa katika kasi na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa pembezoni mwa barabara na
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, mkuu wa Mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti amesema miongoni mwa abiria waliopoteza maisha katika ajali hiyo wanawake ni 5 na wanaume 7. SOMA ZAIDI