IGP Mwema
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Jeshi la Polisi,IGP Said Mwema amefanya
uteuzi wa makamanda wa Polisi kwa mikoa mitatu Mwanza,Mbeya
na Simiyu.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana na Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso ilisema IGP Mwma amemteua Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) Valentino Mlowola kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mwanza.
Pia amemteua Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
(SACP) Ahmed Msangi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Charles Mkumbo kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu.
Taarifa hiyo, ilisema aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, SACP Salum Msangi amehamishiwa makao makuu ya Polisi Dar es Salaam.
IGP Mwema, amemhamisha Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mara, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Ibrahim kwenda Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa Mkuu wa Upelelezi.
Kwa uhamisho huo, nafasi yake inachukuliwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Rogathe Mlasani kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.
Wengine waliohamishwa ni Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam anakweenda kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Martin Otieno kutoka Kanda Maalum ya Dar es salaam, amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi kuwa Mkuu wa kitengo cha Teknohama na Mrakibu wa Polisi (SP) Gidion Msuya ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/ Rorya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tunduru OCD).
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Jeshi la Polisi,IGP Said Mwema amefanya
uteuzi wa makamanda wa Polisi kwa mikoa mitatu Mwanza,Mbeya
na Simiyu.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana na Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso ilisema IGP Mwma amemteua Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) Valentino Mlowola kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mwanza.
Pia amemteua Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
(SACP) Ahmed Msangi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Charles Mkumbo kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu.
Taarifa hiyo, ilisema aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, SACP Salum Msangi amehamishiwa makao makuu ya Polisi Dar es Salaam.
IGP Mwema, amemhamisha Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mara, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Ibrahim kwenda Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa Mkuu wa Upelelezi.
Kwa uhamisho huo, nafasi yake inachukuliwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Rogathe Mlasani kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.
Wengine waliohamishwa ni Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam anakweenda kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Martin Otieno kutoka Kanda Maalum ya Dar es salaam, amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi kuwa Mkuu wa kitengo cha Teknohama na Mrakibu wa Polisi (SP) Gidion Msuya ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/ Rorya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tunduru OCD)