Yelewiii! Dereva ‘suka’ wa kampuni moja binafsi yenye makao yake makuu Kurasini jijini Dar (jina halikupatikana) Jumapili iliyopita alinaswa akifanya mapenzi na changudoa ndani ya gari la kampuni hiyo, kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kilishuhudia tukio hilo laivu.
Dereva huyo akiwa na mwenzake walifika maeneo ya Mbagala Zakhem saa 7 usiku wa Februari 16, mwaka huu bila kujua kama OFM ilikuwa katika maeneo hayo kwa ajili ya kufanya oparesheni tokomeza machangudoa.
OFM ilimshuhudia dereva huyo na mwenzake wakishuka ndani ya gari aina ya Toyota Hilux (isiyokuwa na ‘pleti’ namba upande wa mbele) mali ya kampuni hiyo, wakiingia kwa fujo katika moja ya madanguro maarufu na kupaki gari kisha wakashuka kuelekea kwenye danguro la machangudoa.
Baada ya muda, mmoja wao alirejea akiwa na changudoa maarufu kwa jina la Waluwalu na kujifungia ndani ya gari hilo.
Kama kawaida yake OFM iliwataarifu askari wa Kituo cha Kizuiani waliokuwa doria katika eneo hilo ambao kwa pamoja walilivamia gari na kumuamuru dereva ashuke.
Hata hivyo, suka huyo alikuwa mbishi akaamua kufunga milango na kupandisha vioo ili asiweze kubughudhiwa na kile alichokuwa akikifanya ndani ya gari.
Askari waliokuwa na silaha wakalizunguka gari hilo na dereva huyo alipoona mambo yamekuwa magumu alifungua mlango na kutimua mbio lakini hakufika mbali kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi sambamba na changudoa aliyekuwa naye.
Akizungumza kwa hofu dereva huyo alisema, yeye na mwenzake ni madereva wa kampuni... (jina tunalo) na walikuwa maeneo hayo kwa bahati mbaya na si kama walifika kuwanunua machangu hao.
Dereva huyo alipotakiwa atoe sababu za kujifungia ndani ya gari hilo na changudoa kisha kutoa pleti namba ya mbele ya gari, alijitetea kwa kusema kuwa pleti namba ilidondoka barabarani tangu mchana, hivyo walikuwa wakimtafuta fundi ili awatengenezee.
Alipohojiwa changudoa waliyekuwa naye, hakuwa na lolote la kusema zaidi ya kuangua kilio na kuomba aachiwe huku akilaumu ukali wa maisha kama sababu ya kujiingiza katika biashara ya kujiuza.
Wahusika hao walifikishwa Kituo cha Polisi cha Kizuiani kabla ya kesho yake (Jumatatu) kupelekwa Mahakama ya Jiji kusomewa makosa yanayowakabili.