Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP SUZAN KAGANDA akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la mauaji ya askari Polisi wawili ambao waliuawa wakati wakijitayarisha kukabiliana na Majambazi watatu waliovamia nyumbani kwa mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la IBRAHIMU MOHAMED mkazi wa Ussoke ambapo walipora zaidi ya shilingi milioni moja na laki mbili pamoja na vocha za simu zenye thamani ya shilingi laki moja na ishirini elfu.Kamanda SUZAN alisema majambazi hayo yalikuwa yakitumia bunduki aina ya SMG. |
↧
MAJAMBAZI YAUA ASKARI POLISI WAWILI KWA RISASI
↧