Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

HEMED ATANGAZA RASMI KUMRITHI SHARO MILIONEA, ASEMA YEYE KWA SASA NI MTOTO WA MZEE MAJUTO. SOMA HAPA

$
0
0


Muimbaji na muigizaji na muigizaji wa filamu nchini, Hemedy PHD amesema anaamini amefanikiwa kuziba pengo la marehemu Sharo Milionea aliyeigiza kwenye filamu kadhaa kama mtoto wa muigizaji mkongwe, King Majuto.

Hadi sasa Hemedy ameshaigiza zaidi ya filamu tatu za komedi na Majuto na amesema wametokea kupatana mno kiasi cha kufanya filamu wanazoigiza pamoja zivutie kama zilivyokuwa filamu za Sharo Milionea na Majuto.

“Kwa upande mmoja nimekuwa kama mtoto wake mwingine ambaye nimetokea kumfariji kwasababu mzee napokuwa naye anakuwa na furaha sana na isitoshe tunashare vitu vingi sana,” Hemedy ameiambia Kikwetu Blog.

Hemedy amesema Majuto ameamuamini Hemedy kiasi cha kumwambia kuwa anaweza kuandaa filamu yake mwenyewe ambayo atashiriki kwa mikono yake miwili.

“Kwahiyo itakuwa ni kazi ambayo ipo kibaba na kimwana zaidi kuliko kibiashara zaidi which means ni mzee ambaye anakubali ninachofanya na anaappreaciate sana,” ameongeza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>