Hii inahusisha show iliyofanyika Maisha Club Dar May 4 2014 usiku ambayo Adam Mchomvu ndio alikua mwenye show pamoja na kuzindua video yake mpya ya ‘au sio’ kisha Fid Q ndio akawa MC.Miongoni mwa watu waliokuwa wanapanda kwenye stage kutoa burudani ni kundi la Weusi lakini ilipofika zamu yao kupanda, MC Fid Q hakuwataja kwamba ndio wanapanda kwenye stage bali walipanda kimyakimya.Gossip cop Soudy Brown alizipata stori kwamba WEUSI walikataa kuitwa kwenye stage na Fid Q, yani hawakutaka Fid awataje kwamba ndio wanapanda.
Fid Q alipoulizwa ilikuaje akajibu ‘Zile ni style za show tu mtu anakuja anasema sisi tufanye kama suprise lakini sio kwamba walikua hawataki, mimi na WEUSI tuko poa’
Soudy Brown: Mbona watu wanasema tuzo ulizoshinda ndio zimeleta matatizo?
Fid Q: Hapana na sidhani kama zinaweza kuleta matatizo kwa sababu nina uhakika hata WEUSI wanajua tuzo niliyopewa ninastahili labda kama wao sio hiphop.. hatuna matatizo, hata jana baada ya kuchukua tuzo nilikua kwenye viwanja tofautitofauti na Joh Makini.
Fid Q: Hakujawahi kuwa na tatizo isipokua mashabiki ndio waliwahi kuhisi kuna matatizo, wakati mwingine inabidi uache fans wawe fans.
Baada ya hayo maneno ya Fid Q Soudy Brown alimpata msemaji wa WEUSI ambae ni rapper Nikki wa II aliesema ‘hakuna ukweli kwamba tumekataa kutambulishwa na Fid Q, kama umefatilia show zetu nyingi huwa hatuna utaratibu wa kutambulishwa kwa sababu huwa imezoeleka kila mtu akiingia anatambulishwa, ni kitu ambacho kimezoeleka sana, hata Fiesta yenyewe huwa tunatokea tu bila kutambulishwa’
Kwa kumalizia Nikki wa II amesema labda tofauti iliyopo kati yake na Fid Q ni rasta au majina ila wako sawa na mtu yeyote.
Soudy Brown: Mlipatana lini?
Nikki wa II: ‘Kwani tuliwahi kugombana?’