Mh. Zitto Kabwe akihojiwa na clouds fm amesema kuwa hawezi kukubali au kukanusha kama ni mwanachama wa ACT mpaka hapo kesi ya msingi dhidi ya uanachama wake CHADEMA ifanyiwe maamuzi mahakamani.
Kuhusu kauli aliyosema Dr. Kitila Mkumbo kuwa angetamani Mh.ZZK ajiunge na ACT na kugombea uenyekiti wa chama hicho, Zitto amesema kuwa yeye na na Kitila mkumbo wana mlengo wa siasa unaofanana yaani 'social politics' inayoamini katika maendeleo na maslahi ya jamii kwa ujumla na sio chama wala watu wachache.

Amemalizia kwa kusema kuwa kesi yake pindi ikiisha basi atakuwa wa kwanza kuzungumza juu ya chama alichopo.