Staa wa filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’.
STAA wa filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ amewashukia waigizaji wenzake ambao ni wake za watu na kudai kuwa wanaichafua sanaa hiyo kwa kujirahisisha kwenye ngono na wanaume wengine. Akizungumza kwa sharti la kutowataja majina, Koleta alisema anawatambua wasanii wengi ambao ni wake za watu na hufanya mchezo huo wakiwa eneo la kutengenezea muvi (lokesheni).< “Wananikera, wamezidi kujirahisisha na kufanya uchafu. Kuna baadhi ya wake za watu hawajitambui wakiwa lokesheni na kuishia kufanya umalaya,” alisema.