Askari polisi wa usalama barabarani wa kituo cha polisi kiambu, Linda Okelo ameitwa na kupewa onyo la mwisho na kaimu kamanda wa polisi James Mugeria kwa picha iliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha trafiki huyo akiwa kazini na sare ya kikazi ya sketi fupi anayobana. Kwake imekuwa ni kitu cha kawaida kuvaa sale ya sketi fupi ingawa polisi wengi wa kike wamekuwa wakionekana na sale za suruali
alisema afisa mwandamizi wa polisi wa wilaya.