BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba amemshutumu mzazi mwenziye, Flora Mtegoha, kuwa amekuwa na tabia endelevu ya kumtenga kwenye shughuli za mwanaye.
Akipiga stori na waandishi wetu, alisema anamshangaa mama huyo kumtenga mara kwa mara katika ishu za marehemu mwanaye ambapo alitolea mfano wa maadhimisho ya miaka miwili ya kifo cha mwanaye (Kanumba Day) yaliyofanyika hivi karibuni.
“Huenda wana maslahi yao kuamua kulitumia jina la mwanangu, siwezi kuwazuia lakini watambue kuwa wanakosea sana kwa kufanya hivyo bila kunishirikisha mimi baba yake,” alisema baba Kanumba.