Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

MAPENZI YA JINSIA MOJA (USAGAJI) YAZIDI KUSHIKA KASI KWA WANAWAKE WA KITANZANIA-DIDA MTANGAZAJI WA RADIO TIMES FM NAYE YEMEMKUTA SOMA HAPA

$
0
0
DUNIA ina mambo! Prizenta wa Radio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ amezua timbwili baada ya kung’ang’aniwa na mwanamke mwenzake aliyedaiwa kutaka kumshawishi afanye naye mapenzi ya jinsi moja (usagaji).
Prizenta wa Radio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’
Dida alikumbwa na ishu hiyo, Alhamisi ya wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar, wakati Kundi la Mashauzi Classic, lilikuwa likiangusha burudani.
Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu, mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina moja la Addy ambaye anadaiwa kukubuhu kwa tabia hiyo chafu ya usagaji.

Ilisemekana kwamba mwanadada huyo alianza kumzengea Dida kwa kumsemesha huku akimuonesha pozi za kimahaba.
Dida akiwa mzigoni ndani ya ofisi za Times Fm.
Licha ya mtangazaji huyo kumpuuza, Addy alifika mbali na kuanza kumshtua kwa kutokea nyuma yake kwa kumtekenya huku akimkonyeza na kumshawishi waongee vizuri.
Kutokana na vitendo hivyo, Dida alipandwa na hasira na kuchukua chupa kutaka kumpasua ndipo Addy naye akawa anahangaika kujitetea na kusababisha vurugu katika eneo hilo, shukrani ziwaendee wasamaria wema waliwatuliza.
Akizungumza na Risasi Jumamosi mara baada ya kutulizwa, Dida alisema:
“Huyu dada ni muda mrefu alikuwa akinisumbua hapa ukumbini, mwanzo nilikuwa sijajua anachotaka kumbe ni mshenzi kabisa, anataka kunifanya vitendo vya kisagaji, amenikera sana.”

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles