MWENYEKITI wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Stive Nyerere’ ameibuka na kumuonya Wema Sepetu kupiga kazi na kuepuka umaarufu bila kazi.
Nyerere amemtaka Wema aachane na skendo za kila kukicha kwani hazina maana kama kazi ya sanaa aliyoichagua kama njia ya kumuingizia kipato.
Wema Sepetu akiwa na Diamond Platinum.
Wema Sepetu akiwa na Diamond Platinum.
“Kwanza nampongeza sana Diamond kwa tuzo zote alizopata kwa kuwa alistahili lakini Wema naye anapaswa kuiga mfano, vinginevyo atakuwa maarufu bila ya heshima,” alisema Steve Nyerere.