Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mapema Machi mwaka huu alikabidhiwa nishani ya kumbukumbu ya Profesa M.O. Oyawoye aliyewahi kuwa Profesa wa kwanza duniani kutoka Bara la Afrika katika masuala ya jiolojia huko nchini Nigeria. Profesa Muhongo alikabidhiwa nishani hiyo na timu ya wanajiolojia kwa kutambua mchango wake mkubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla. Nishani hiyo alikabidhiwa balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay kwa niaba yake.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa ofisini kwake huku akiwa amevaa nishani hiyo.