Msanii wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha.
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha na meneja wake, Joe Kariuki wanatarajia kufunga ndoa Novemba, mwaka huu nchini Kenya jijini Nairobi.Akizungumza na mapaparazi wetu, Meneja wa Baby Madaha, Joe alithitisha mipango hiyo na akasema sasa wanafanya kazi nyingi za muziki mpaka zifike nyimbo 20 ambapo baada ya kuoana zitaanza kutoka mojamoja kwa muda wa miaka minne.
Baby Madaha akiwa katika moja ya kazi zake na meneja wake,Joe.
“Ni kweli tumepanga kuoana, kikubwa ninaandaa nyimbo nyingi ili baada ya ndoa nitasimama muziki na badala yake nitakuwa naachia nyimbo tu,” alisema Baby anayetamba na Wimbo wa Nawaponda.