Kuiga ni kawaida kwa wengi.Wapo walioiga mambo fulani na hatimaye wakafanikiwa, na pia wapo walioiga vitu flani wakaharibikiwa.Huyu aliiga na akaharibu kila kitu...
Ni msanii wa siku nyingi katika fani.Alitamba zaidi akiwa Kaole, na hata mwanzoni mwa ujio wa filamu za Kanumba alizidi tu kashaini....
Kiasili ni mweusi japo siku hizi kuna weupe fulani katika ngozi yake nyororo.Ana sura nzuri yenye mvuto,umbo aslia la kibantu,meno yake meupe yamepambwa na mwanya mdogo na kufanya iwe fahari kumuona akitabasamu...
Hana kashfa ya kuvaa nguo fupi sana ila aliwahi kukumbwa na skendo kubwa zaidi.Mkumbuke vizuri.Mrefu wa wastani,anajua kutembea,anaongea kwa mapozi huku akipenda kulamba papi ya midomo yake. Umemjua???....Hapana, siyo huyo...!!
Huyu ni mpole kiasili na anapendwa sana na mama yake.Katika maigizo ana uwezo wa kukufanya uamini unachoangalia ni kitu halisi.Japo huwezi kumtaja, ila ndani ya wasanii kumi anapaswa kuwamo...
Na ingawa mvuto wake umepungua kiasi,ila bado mrembo sana.Lakini wakati anaigiza Kaole alikuwa mrembo zaidi.Kwa uzuri wake , alivuma na kila habari inayohusu mwanaume maarufu na mwenye pesa
Habari ya kutakiwa na kila mwanaume , wenye rangi na vipato tofauti zilisikika kila kona.Baadhi alitoka nao na wengine haikuwa bahati yao....
Toka kitambo almanusura aolewe, ila ni miaka ya juzi juzi ndipo aliolewa.Uzuri wake si wa kutafuta, kila mwenye macho na ngozi ya kuhisi atautambua....
Mbali na majanga yote aliyopitia katika maisha yake,mengine yakibaki kumchafua na watu kudhani hawezi kuolewa na mwanaume yeyote kabla ya ile bahati ya mtende akaolewa; yeye aliamua kuachana na ndoa yake kwa kuona aishi katika umaarufu wake....
Mara kadhaa alikuwa akiwaambia marafiki zake kuwa, mwenye hadhi na anayetakiwa kuishi kama Wema Sepetu sio Wema bali ni yeye na wakongwe wengine waliosotea sanaa na kuipigania kama roho zao na kuilinda kama mboni ya jicho lao.....
Akaona ndoa sio mahala pake,bila sababu za msngi akaamua kumwambia mumewe watengane....Japo haikuwa rahisi ,lakini walitengana!!
Cha kufurahisha ni kwamba bado Wema anaishi kama Wema na bado yeye haishi kama Wema Sepetu na ndoa haipo tena...Umemjua ninayemzungumzia?