Mwili wa Dk. Raymond Simion ukitolewa kwenye chumba cha kulala wageni na polisi.
MTU mmoja aliyedaiwa kuwa ni daktari wa jijini Mwanza, Raymond Simion (36) amekutwa amekufa ndani ya chumba kwenye nyumba ya kulala wageni ‘gesti’ ijulikanayo kwa jina la Nesta iliyopo Ubungo NHC wilayani Kinondoni jijini Dar.Taarifa kutoka katika gesti hiyo zinasema marehemu alijiorodhesha kwenye kitabu cha wageni kuwa ni daktari wa Hosptali ya Nyamagana jijini Mwanza na alikuja Dar kikazi kwa muda wa wiki moja. Mauti yalimkuta akiwa na siku mbili tu tangu alipowasili.
Mmoja wa wahudumu wa gesti hiyo ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini alisema kuwa, daktari huyo alifika katika gesti hiyo Jumapili ya Mei 4, mwaka huu na kuchukua chumba namba 102.
Alisema Jumatatu ya Mei 5, marehemu aliomba abadilishiwe chumba, akapewa namba 105 ambamo mauti yalimkutia.
Alisema Jumatatu ya Mei 5, marehemu aliomba abadilishiwe chumba, akapewa namba 105 ambamo mauti yalimkutia.
Uwazi lilifanikiwa kufika katika eneo la tukio na kufanya mahojiano na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ubungo NHC, Amani Sizian ambaye alisema taarifa ya kifo cha daktari huyo aliipokea saa 9: 03 alasiri ya siku ya tukio ambapo mhudumu wa gesti hiyo ndiye aliyempigia simu kumjulisha.INAENDELEA>>>>>>