Mchungaji Mary Izengo.
MARY Izengo (52), mkazi wa Kijiji cha Umanda- Msalala, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza anateseka kiasi cha kutamani afe kufuatia gonjwa la ajabu alilonalo huku akisema ndugu, wakiwemo watoto wake wamemtenga.
Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Wadi Namba 23, Jengo la Sewa Haji kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, mwanamke huyo alisema usiombe gonjwa hilo likupate kwani ugonjwa unaomkabili ni wa uvimbe mkubwa usoni ambapo unamtesa kwa kipindi kirefu huku akionekana kero kubwa katika jamii.
ATOA HISTORIA YAKE HUKU AKILIA
Hata hivyo, mwanamke huyo ambaye wakati akizungumza na Uwazi mara kwa mara alikuwa akilia, alisema:“Nilizaliwa mwaka 1962 katika Kijiji cha Umanda Msalala, wilayani Sengerema nikiwa mzima wa afya wala sikutegemea kama siku moja ningekuja kuwa katika hali hii.
“Nikiwa na umri wa miaka mitano ndipo nilipoanzwa na tatizo hili. Ulianza kwa kutoka vipele vidogovidogo mdomoni ambavyo viliniletea maumivu makali. Wazazi walinipeleka hospitali nikatibiwa kwa kuchomwa sindano lakini bila mafanikio.INAENDELEA>>>>>>