MARY Izengo (52), mkazi wa Kijiji cha Umanda- Msalala, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza anateseka kiasi cha kutamani afe kufuatia gonjwa la ajabu alilonalo huku akisema ndugu, wakiwemo watoto wake wamemtenga.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Wadi Namba 23, Jengo la Sewa Haji kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, mwanamke huyo alisema usiombe gonjwa hilo liliompata akiwa na umri wa miaka 5 likupate kwani ugonjwa unaomkabili ni wa uvimbe mkubwa usoni ambapo unamtesa kwa kipindi kirefu huku akionekana kero kubwa katika jamii.
Mary aliendelea kusema kuwa, siku moja alijikuta akisukumwa kwenda kwenye mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Nyang’wale wilayani Geita, Mhe. Ahmed Nassor Amar ‘Gulamali’.
alisema mama huyo.
Mary anaomba msaada ili aweze kupata fedha zitakazomuwezesha kwenda India kutibiwa. Ukitaka kumsaidia tuma fedha kwa namba 0683 406 680 ya afisa ustawi wa jamii aliye karibu naye.