Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

DAVIDO AIINGIA MATATANI KWA HIKI KITENDO ALICHOKIFANYA

$
0
0

davidoAnaitwa Davido Adeleke lakini kwenye muziki tunamjua kama Davido na yeye anajitambulisha na a.k.a yake maarufu Omo Baba Olowo (O.B.O).


Labda tatizo linalomkuta Davido ndilo lile lile kama kwa Chris Brown na Justin Bieber, kuwa na pesa nyingi na umaarufu akiwa na umri mdogo.


 Akiwa kwenye harakati zake za kwenda kwenye show uingereza Davido alifika airport na passport yake ya Marekani.Maafisa wakamwambia alete passport ya Nigeria kwasababu passport hiyo ya Marekani haikuwa na karatasi za visa ya kuingia Nigeria kwa hiyo utaratibu haujafuatwa.

 dsdd
 Davido alisisitiza kwamba anayo passport ya Nigeria lakini ameiacha nyumbani. Hakuruhusiwa kusafiri hadi hiyo passport ya Nigeria ilivyoletwa na akaruhusiwa kusafiri. Baada ya hapo ali-tweet akiwatusi maafisa wa hapo airport kwa kile kilichotokea.
 
daviOfisi ya maafisa wa uhamiaji wamesema tabia kama hiyo ya bwana Davido Adeleke sio sawa kabisa kwasababu afisa huyo alifata utaratibu wa kazi ambao umesaidia Davido. 

Huko mbele ya safari angeweza kurudishwa au kuaibika zaidi kwani kwenye airport nyingine ambapo utaratibu unafatwa kwa hali ya juu wasingemruhusu kuendelea na safari.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles