Wabunge kutoka eneo linalokuza mmea wa Khat au Miraa la Meru mashariki ya Kenya wametishia kuwasilisha mswada bungeni kulazimisha serikali kuwafukuza wakulima waingereza wanaoishi katika eneo hilo.
Hii ni baada ya bunge la juu nchini Uingereza kupiga kura na kuidhinisha sheria inayoweka marufuku ya kuingizwa mmea huo nchini humo kutoka Kenya.
Waziri wa mambo ya ndani nchini Uingereza, Theresa May amekuwa akipigia debe marufuku hiyo akisema kuwa Miraa ni mmea unaolewesha kama dawa zingine za kulevya.
Wabunge hao wanasema kuwa wamejaribu mbinu zote za kisheria na kidiplomasia kushawishi Uingereza kutoharamisha Miraa kutoka Kenya ingawa wamekosa kufaulu.
Wakulima wa Meru hukuza sana Miraa kama kilimo cha kuwapa mapato
Kadhalika Wabunge hao wanasema kuwa hatua ya kupigwa marufuku mmea huo itasababisha karibu watu milioni mbili kukosa ajira.
Mapema wiki hii bunge la malodi nchini Uingereza liliidhinisha marufuku dhidi ya Miraa mapema wiki hii huku waziri wa maswal ya ndani akionya kuwa kukosa kuharamisha Miraa ambayo inasemekana kuwa katika kiwango sawa cha madawa ya kulevya m uingereza itageuka kuwa eneo la kufantyia biashara haramu ya mmema huo.
Miraa hutumiwa sana na jamii za watu wa Yemen na wasomali nchini Uingereza.
Marufuku hiyo ndio chanzo cha hasira miongoni mwa wakulima wa Kenya wanaokuza mmea huo ambao wabunge wao wanaitaka serikali ya Kenya kuwafukuza wakulima waingereza wanaomiliki mashamba katika eneo hilo.
Wanasema kuwa mashamba yao hutumiwa kukuza Miraa na hayawezi kutumiwa kuapnda chakula kingine. Pia wabunge hao wanasema kama marufuku hiyo ipo kweli basi wakulima wapewe mashamba mengine ya kupanda chakula.
Wakulima waingereza wanamiliki karibu robo ya mashamba katika eneo la Meru wakipanda wimbi.