MSANII wa filamu, Halima Yahaya ‘Davina’ amekunwa na maneno ya Mheshimiwa Felix Mkosamali, Mbunge wa Muhambwe mkoani Kigoma aliyoyatoa juzi bungeni ya kutaka serikali iweke mikakati madhubuti ili kulinda haki za wasanii wa filamu nchini.
Akizungumza na Ijumaa juzi Davina alisema, amejisikia faraja sana kuona kiongozi huyo anaumizwa na jinsi wanavyonyonywa kisanii hivyo akawataka wengine kulipigia kelele suala hilo ili wasanii waweze kuneemeka.
“Maneno ya Mheshimiwa Mkosamali yamenipa faraja sana, naamini tunakoelekea ni kuzuri kwa kuwa naamini serikali yetu ni sikivu na haiwezi kunyamaza kuona tunanyanyasika wakati kazi tunayoifanya ina faida kubwa kwa taifa,” alisema Davina.