Ajali mbaya imetokea muda mchache uliopita katika lango Kuu la kuingilia katika Mahakama ya mjini Tabora. Ajali hiyo imehusisha Gari ndogo aina ya Rav 4 yenye usajili wa namba T516 ALA ambayo ilikuwa inaendeshwa na Mama mmoja aliye tambulika kwa jina la Stumai Tambwe ambapo ameigonga Bodaboda iliyokuwa na Abiria na kuwasababishia kuumia vibaya san, na baada ya hapo Gari hilo liligonga mti na kumsababishia kuumia vibaya.
↧