Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

PICHA ZA UTUPU SI MCHEZO

$
0
0

Tunaendelea kupata mtiririko wa mahojiano ya mwingizaji Nuru Nasoro ‘Nora’ tuliyoanza wiki iliyopita, karibu: 

Mwigizaji mkongwe wa tasnia ya filamu za kibongo Nuru Nasoro ‘Nora’
Gladness: Unawaambia nini wenzako wenye tabia hizo chafu za kutembea na watu ovyo?
Nora: Mimi nawaasa waachane na tabia hiyo kwani magonjwa ni mengi ukizingatia kuwa wanaume wenyewe wanawatumia tu kama vyombo vya starehe.
Gladness: Ni kitu gani ambacho kimewahi kukuumiza sana katika maisha yako?
Nora: Ukweli picha za utupu ziliniumiza sana kwani zilikuwa ni mbinu za wasanii wenzangu kutaka kunishusha kisanaa ambapo walinipiga nikiwa nimelala sijielewi.
Gladness: Huwa unaenda msikitini?
Nora: Ndiyo, mara mojamoja kwani mara nyingi huwa naswali nyumbani kwa siku mara tano.
Gladness: Kwa nini msikitini mara mojamoja?
Nora: Dini yetu inaruhusu mwanamke kuswali nyumbani kwani ndiyo anapata thawabu zaidi.
Gladness: Uliwahi kuwa na bifu na Vincent Kigos ‘Ray’ na Blandina Chagula ‘Johari’, je kwa sasa mkoje?
Nora: Mimi nilishawatangazia msamaha kwa yote mabaya waliyonitendea, Johari huwa tunaongea lakini Ray sijawahi kuongea naye.
Gladness: Zamani uliwahi kuwa kichaa na kupotea kabisa kwenye fani, je unayazungumziaje maisha hayo ya nyuma?
Nora: Huwa sitaka kuyakumbuka kwa sababu yananisikitisha sana, nilipoteza muda mwingi sana na kurudishwa nyuma kimaendeleo.
Gladness: Ni mafanikio gani uliyoyapata kwenye sanaa mpaka sasa?
Nora: Sijapata mafanikio yoyote zaidi ya kujulikana kwa sababu sanaa ya Tanzania bado iko nyuma, hailipi kihivyo kama watu wanavyofikiria.
Gladness: Nini sababu za kuachana na mume wako wa kwanza, marehemu Ng’wizukulu Jilala?
Nora: Huwa sipendi kuzungumzia sana hilo ila kilichosababisha mimi kuachana na mume wangu wa kwanza ni kwamba alikuwa akinitesa sana yaani nilikuwa nashushiwa kipigo kila kukicha.
Gladness: Je, ulipewa talaka au uliamua kuondoka tu mwenyewe?
Nora: Ukweli baada ya kuona mateso yamenizidi niliomba talaka mwenyewe lakini aliitoa kwa nguvu baada ya wazazi wangu kuingilia kati.
Gladness: Ulifanikiwa kuzaa naye watoto wangapi?
Nora: Nilifanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja tu ambaye ndiye niliye naye mpaka sasa.
Gladness: Tuachane na mume wa kwanza tuje kwa huyu wa pili (Luqman), nataka kujua je, yeye hukufanikiwa kuzaa naye?
Nora: Hatukufanikiwa kuzaa, nami sikuwa tayari kuzaa naye kwa sababu kuna vitu ambavyo vilikuwa havijatimia.
Gladness: Baada ya kuachana na Luqman uliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzako Geofrey na mliahidi kwamba mtaoana lakini mkaachana, nini sababu?
Nora: Mimi sikuwahi kuwa na uhusiano na Geofrey yule alikuwa ni meneja wangu na tulikuwa tukishirikiana katika kazi.
Gladness: Je kwa sasa una mchumba au mpenzi?
Nora: Sina mpenzi wala mchumba.
Gladness: Wewe ni mwanamke uliyekamilika unawezaje kuzuia tamaa za mwili wakati hauna mpenzi?
Nora: Huwa ninafanya mazoezi sana hivyo naweza kuzizuia tamaa hizo za mwili.
Gladness: Je una mpango wa kuzaa tena?
Nora: Ndio, nikishaolewa nitazaa lakini siwezi kuzaa nje ya ndoa.
Gladness: Je unahitaji mwanaume wa aina gani?
Nora: Namuhitaji mwanaume atakayenipenda mimi Nuru na siyo Nora, mwenye mapenzi ya kweli, atakayeniweka mimi mbele kwenye kila jambo, anayejishughulisha kimaisha, mtanashati na anayemuogopa Mungu.
Gladness: Turudi nyuma kidogo kwenye kipindi ambacho uliugua sana na kuwa kichaa, je ni wasanii gani waliokuwa bega kwa bega na wewe?
Nora: Hakuna hata mmoja aliyekuja hata kuniona zaidi walikuwa wakinikandamiza.
GPL

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>