Kwa kawaida kila Tuzo zinataratibu zake na njia zitakazowafanya watu washinde . Tuzo kama Oscar Awards au Grammy Awards hupata washindi kwa kutengeneza team ya wadau mbalimbali na kuiita Academy. Ndani ya hawa members wa Academy ndio mshindi hupatikana.
Kwa tuzo za BET nayo itakua hivihivi huku kukiwa na Academy Members 500 kutoka dunia nzima, washindi wa categories zote watachaguliwa na hawa members, kwa hiyo kura yako haitahusika kwenye tuzo za BET , lakini usijali sababu bado utamuwezesha Platnumz ashinde tuzo za ChannelO na MTVBase. Cha kufurahisha lakini katika tuzo za BET ni kwamba mmoja wa majaji hao 500 ni muimbaji , Vanessa Mdee kutoka Tanzania.