Huku akiwa anasuburia kunyakuwa tuzo za MTV zinazotarajiwa kufanyika tarehe 7 june, Diamond amechaguliwa kuwania tuzo za BET katika category ya "Best International Act (Africa)
Diamond anachuwana na mwanadada Tiwa Savage (Nigeria), Davido (Nigeria), Mafikizolo (South Africa), TOOFAN (Togo) na Sarkodie (Ghana)
Diamond anasema hakutarajia kabisa kama angechaguliwa katika tuzo hizo kwasababu hajawahi kuwasiliana nao hata siku moja. Akiongea kutoka London amesema wakati yuko set akiendelea na ku record video yake mpya, manager wake Babu Tale ndio alimwambia amechaguliwa BET ila akadhani ni utani , ila baada ya kuona tweets nyingi za mashabiki ndio akaamini. INGIA HAPA