Gari aina ya RAV4 ikiwa chali baada ya
Kupata ajali mbaya Maeneo ya Kibaigwa ukiwa uanelekea Mkoani Dodoma.Mh:Mwigulu Nchemba akisaidia kuoka Majeruhi kwa Kuinua gari.
Gari aina ya RAV4 ikiwa imeshainuliwa tayari na Majeruhi wametoka walikuwa wawili.Kazi ya Kuondoa Betri ya Gari ndio inafanyika ilikuepusha Moto.Huyu ndiye alikuwa Dreva wa gari hii iliyopata ajali,amepata Michubuko kidogo.

Ajali ndogo Imetokea maeneo ya Kibaigwa ikihusisha gari aina ya RAV4 iliyokuwa ikitokea Mkoani Morogoro kwenda Dodoma,Ajali hiyo mbayo haijasababisha Kifo chochote imetokea majira ya Mchana wa Tar.08/06/2014 na Sababu ya ajali inatajwa kuwa ni Mwendo kasi wa Dreva na hatimaye Gari Kumshinda na kupinduka.
Katika tukio hilo Mh:Mwigulu Nchemba aliyekuwa akitoka Dodoma kuelekea Morogoro kwenye Mkutano alilazimika Kusimama kwa Muda kwenye ajali hiyo kwaajili ya Kutoka Huduma ya Kwanza kwa Majeruhi kama anavyoonekana Pichani hapo Juu.Jambo hilo liliwafurahisha sana Wananchi waliokuwa eneo la ajali na waliomba Viongozi wengine waige tabia hii ya Mwigulu Nchemba ya Kushirikiana na Wananchi wakati wa Shida husuasani wanapoona ajali barabarani,Ugonjwa,Misiba n.k wajitahidi kutoa Ushirikiano.