Jana Jumapili ya tar 08.06.2014 ulifanyika uzinduzi wa ukumbi mpya mjini Dodoma uliopo maendeo ya Stendi ya mkoa ambapo ilikuwepo Bendi mpya ya Malaika au Wafalme wa Masauti waliotoa burudani kali mbele ya mashabiki wao kibao waliojitokeza kufurahi jioni
…
Tazama picha mbalimbali watu wakila burudani mwanzo mwisho.
Andrew Sekedia alitekenya kinanda vya kutosha kuwapagawisha mashabiki
Wafalme wa Masati hapa wakilikamua Sebene ipasavyo
Christian Bella akikamua sambamba na wanamuziki wenzake
Mashabiki walishindwa kukaa kwenye viti kiasi cha kusogea na kulisakata Rhumba kali zilizokuwa zikishushwa toka kwa Wafalme wa masauti
Christian Bella akiwaimbisha mashabiki wimbo wake mpya wa Mama
Hapa wanenguaji nao walifanya yao sambamba na Rapa wa bendi hiyo
Dj Kipaso toka Dodoma Carnival nae aliongea yake machache
Mkurugenzi wa Dodoma Carnival alitoa yake machache na kuwakaribisa watu wote wa Dodoma kufika pale kwani ndo kiwanja kinachokimbiza kwa sasa hapa Dodoma.
Shabiki alipanda jukwaani kuonesha uwezo wake…ilikuwa ni shiiiiiiiidaaaaa……
Shabiki Elibariki au Osama Mweusi kama alivyopewa jina hilo hapo jana alipanda na kuonesha yake.
Boss Ngasa nae alikuwepo