HII ni kali lakini haikuwahi kuandikwa, staa wa Bongo Fleva, Ally Timbulo alinusurika kuuawa baada ya kubainika kuwa anatembea na mke wa mtu na mumewe kumsaka kwa udi na uvumba akiwa na bastola mkononi.
Akitema cheche na Untold, Timbulo alisema, katika maisha yake hakuwahi kufikiria kutoka kimapenzi na mtu ambaye yupo kwenye ndoa, isipokuwa mwanadada huyo ambaye anafanya kazi serikalini (jina kapuni) alionesha upendo wa dhati kwake pamoja na kumgharamia kwa kila alichohitaji.