Inauma sana! Zikiwa zimekatika takriban siku 18 tangu alipofariki dunia aliyekuwa staa wa sinema za Kibongo, Sheila Leo Haule ‘Recho’ (26) na mwanaye, imefahamika kuwa mzimu wake bado unamtesa mumewe, Saguda George.
Nyumba aliyopangisha Saguda na marehemu Recho Haule ambayo walilipia kodi ya shilingi milioni tatu iliyoko maeneo ya Sinza-Kwaremy, Dar.
Habari zilieleza kwamba kabla ya kukutwa na umauti Mei 27, mwaka huu, Recho alikuwa amepangisha nyumba aliyokuwa anahamia kwa ajili ya malezi ya mwanaye na uzazi kwa jumla.
Ilifahamika kuwa nyumba hiyo aliilipia kodi ya zaidi ya shilingi milioni tatu ambayo ipo maeneo ya Sinza-Kwaremy, Dar.
Ilifahamika kuwa nyumba hiyo aliilipia kodi ya zaidi ya shilingi milioni tatu ambayo ipo maeneo ya Sinza-Kwaremy, Dar.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, mbali na kupangisha nyumba hiyo, pia Recho alifanya shopping ya vitu mbalimbali vya mtoto kama nguo, midoli na vinginevyo vinavyohitajika wakati wa kulea mtoto.
Ilisemekana kwamba Recho alivipeleka vitu hivyo nyumbani alikokuwa akiishi na Saguda maeneo ya Kinondoni, Dar hivyo kumpa mumewe wakati mgumu kila anapovitazama vitu hivyo.
Ilisemekana kwamba kila akivitazama vitu hivyo hulikumbuka lile jeneza dogo la mwanaye na mkewe pia na kujiona kama anaota.
Ilisemekana kwamba kila akivitazama vitu hivyo hulikumbuka lile jeneza dogo la mwanaye na mkewe pia na kujiona kama anaota.
Kuhusu nyumba aliyolipia Recho, ilisemekana kwamba Saguda ‘ameikimbia kwani kila akienda kwenye nyumba hiyo amekuwa akikutana na mzimu wa mkewe huyo.
Aliyekuwa mume wa Recho (Saguda) akilia kwa uchungu wa kuondokewa na aliyekuwa mpenzi wake Recho Haule.
Ilielezwa kuwa Saguda alifikia hatua hata ya kusamehe fedha hizo (zaidi ya shilingi milioni tatu za kodi) kwani hawezi kuishi kwenye nyumba hiyo na kwamba kama atapatikana mpangaji mwingine bora aingie.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, tulimsaka Saguda ambaye ni bonge la cameraman na mwandishi wa miswada ya filamu za Kibongo.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, tulimsaka Saguda ambaye ni bonge la cameraman na mwandishi wa miswada ya filamu za Kibongo.
Saguda alipopatikana alisema kuwa, baada ya kuondokewa na mpenzi wake amekuwa akiishi kwa tabu kwani kila akitazama vitu alivyokuwa akivitumia Recho anauona mzimu wake na kujikuta akilia.
“Hanitoki, hata nikifumba macho sura yake hainitoki machoni. Nilimpenda sana Recho, nampenda na nitampenda siku zote pamoja na kwamba sipo naye kibinadamu lakini kiroho tupo pamoja kwa sababu tulipendana sana,” alisema Saguda kwa maumivu makali.