Kutia alama mwilini umekuwa utamaduni kwa miongo kadhaa katika maeneo tofauti barani Afrika ili kuashiria urithi wa kikabila.Vitendo hivi hata hivyo vinapungua lakini bado kuna watu wanaotaka kuendeleza kilichofanya na mababu zao.Katika mji wa Ouidah kaskazini mwa Benin, kuna tambiko inayotarajiwa kufanyika ikifuatwa na siku mbili za sherehe.Houeda ni mojawapo wa makabila nchini Benin inayoamini kuwa tendo la kuchanja watoto – hasa usoni- huwaunganisha na mababu zao.
Watoto hao hupewa majina mapya, wananyolewa vichwa vyao na kupelekwa katika makazi ya watawa ambapo kuna mizimu inayowasaidia kuzungumza na vizazi vya hapo awali.
'Utamaduni unaoenziwa'
“Hii ni sehemu ya tamaduni zetu na ni muhimu sana kwangu,” anasema Genevieve boko, ambaye mwanawe wa kike mwenye umri wa miezi 6, Marina, pamoja na wapwa zake Luc na Hospice wenye umri wa miaka 10 na miaka 12 wote wako tayari kuchanjwa.
Mpekuzi ilifanya mahojiano na mama huyo ambaye naye alionyesha kushangazwa na tukio hilo na kusema hajui tatizo lililomfanya ajifungue mtoto huyo kwa kuwa hakuwahi kusikia maumivu ya aina yoyote wakati wa ujauzito huo hadi alipofikia hatua ya kujifungua….
Katika mahojiano hayo, mama huyo alisema kuwa huo ni uzao wake wa 6 na hajawahi hudhuria Clinic
Jivu hutumika kutia alama sehemu ambayo chanjo hiyo hufanywa na huchukua sekunde chache chanjo hiyo kufanya.
“Rafiki zangu waliniuliza iwapo ni uchungu na iwapo nililia na nikasema ‘la!’,” alisema Luc baadae. “Kabla, nilipokuwa
nikitembea mitaani pamoja na ndugu yangu mkubwa aliye na makovu, watu hawangeamini kuwa ni ndugu yangu. Sasa nina furaha kwa kuwa tunafanana.”Tangu mume wake alipoaga dunia, Gamba Dahoui amekuwa akifanya chanjo zote za nyumbani-anasafisha vifaa vya kuchanjia kwa mimea yenye dawa pamoja na tembo. Makaa pia huwekwa kwenye majeraha ili kuyasaidia kupona.
Dahoui hutumia kisu kimoja tu kila wakati, huku akipuuza mashari rasmi ya kutumia nyembe safi kwa kila mtu ili kuepuka hatari ya kuambukiza magonjwa yanayoambukizwa kwa damu kama vile pepopunda na UKIMWI.Chanjo hizi hata hivyo zimeanza kupoteza umaarufu. Idadi kubwa ya familia inashiriki sehemu ya kwanza tu ya sherehe hizo, na kuacha kabla ya chanjo kufanywa.Ni sawa sawa na sehemu mbalimbali ya taifa hilo ambapo kila kabila huwa na mfumo wake wa kuchanja.
'Ni aibu kukosa alama au makovu'
“Nikiwa na makovu yangu, ninatambulika kila mahali ninapokwenda,” anasema Fleury Yoro, anayeishi Atacora, kaskazini mwa taifa hilo. “Iwapo ningepata nafasi ya kufanya uamuzi, singependa kuwekewa makovu namna hii.”
Anasema kuwa alipokuwa akisoma katika jiji kubwa zaidi nchini Benin Cotonou, alikejeliwa mara kwa mara kutokana na makovu yake. Watu kadhaa ‘‘hawangependa watu wengine wadhani kuwa walikuwa marafiki na mtu mshenzi namna ile,” anasema.Wengine wana maoni tofauti ya kufanya uamuzi wa kutochanja vizazi vichanga. Sinkeni Ntcha aliacha kitendo hicho baada ya watoto wake 3 wa kwanza ‘‘kwa sababu ya UKIMWI,” anasema. ‘‘Nyembe zinapaswa kubadilishwa kila wakati lakini wakuu walikataa.”Kwake, kama mmoja kati ya watu wa kabila la Otomari, alama hizo “hazina maana”. Utamaduni unawezwa kuendelezwa kwa njia nyingine, anasema, kupitia kwa lugha, densi, unyago na usanifu.Watu wengi wa kabila la Otomari bado wanakubali kutiwa alama, wakiwemo wanawake kadhaa wachanga ambao wakati mwingine huchanjwa kwenye migongo yao na tumboni wanapobalekhe ili ‘‘kuonyesha ujasiri wako,” anasema Edith (aliyeonyeshwa kwenye picha). Mifumo huwa sawa mara kwa mara na michoro inayochorwa kwenye mijengo ya mitaani.
Wakati mwanawe Genevieve Boko, Marina (hapo chini) alipokuwa na umri wa miezi 6 tu alipotiwa alama – watoto katika sehemu zingine nchini Benin hufanyiwa kitendo hicho juma moja tu baada ya kuzaliwa.
Katika nchi jirani ya Nigeria, suala la haki za watu wachanga limesababisha baadhi ya majimbo kupiga marufuku zoezi hilo kwa watoto wote.
Katika nchi jirani ya Nigeria, suala la haki za watu wachanga limesababisha baadhi ya majimbo kupiga marufuku zoezi hilo kwa watoto wote.
Hata hivyo, hii sio hatua inayowapendeza watu wote wa Benin. ‘Hatukiuki haki za watoto, tunawaonyesha watoto walikotoka na kile watakachopitia maishani,” anasema Telesphore Sekou Nassikou, mhariri mkuu wa kituo kimoja cha redio mjini Natitingou iliyoko kaskazini magharibi mwa taifa hilo.Kwake, makovu hayo hupitisha ujumbe: ‘‘Tahadhari, kuna uchungu katika dunia hii, na utahisi uchungu katika maisha yako. Hata hivyo uchungu huo utaisha iwapo utavumilia.”