Mama mzazi akiwa na Mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya msingi Motomoto kata ya Vumilia wilayani Urambo aliyekatwakatwa mapanga na mfanyakazi wa nyumbani kwa madai ya kunyimwa hela na baba mzazi wa mtoto hu
======== ======= =======
Na Allan Ntana, Urambo
MTOTO Perezi Christian (12) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Motomoto iliyoko katika kata ya Vumilia wilaya ya Urambo mkoani Tabora amekatwakatwa mapanga mikononi na miguuni na mfanyakazi wa nyumbani.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa akiwa wodini alikolazwa Perezi mama mzazi wa mtoto huyo Regina Fumbo (45) ambaye ni muuguzi katika kituo cha afya Zogolo kilichoko katika tarafa ya Nyasa wilayani Nzega alisema mtoto wake amekatwakatwa mapanga na mfanyakazi wa shambani anayeitwa Abdallah Alfan muha mwenye umri wa kati ya miaka 39-44.
Alisema awali hapakuwa na ugomvi wowote kabisa kila alichotaka alikuwa anapewa, alichukua uamuzi huo kwa hasira tu kwani tayari alikuwa ameahidiwa kulipwa hela alizokuwa ameomba kwa bosi wake ambaye ni baba mzazi wa mtoto huyo Bw. Christian Mlela.
‘Hili tukio limenisikitisha sana, nilipigiwa simu nikiwa kazini kwangu kule Nzega, nikajua mtoto wangu sitamkuta hai tena, nilikuja mbio mpaka wodi ya wanaume alipolazawa, kwa kweli hali yake haikuwa nzuri, namshukuru Mungu sasa hivi anaendelea vizuri, na huyo mtuhumiwa ameshakamatwa na polisi’, alisema.
SOMA ZAIDI >>>>.