Marekani imeiwekea Uganda vikwazo kwa kupitisha sheria zinazopinga mapenzi ya jinsia moja katika taifa hilo.Inasema vikwazo hivyo vitajumuisha marufuku ya wanaharakati waliopigia debe sheria hiyo kupitishwa kutoingia Marekani.
Ikulu ya nchi hiyo pia imesema itapunguza misaada kwa miradi kadhaa inayofanya kwa msaada wa Marekani kwa mamlaka za Uganda na kufuta mazoezi ya kijeshi kati ya Uganda na Marekani.
Uganda imesema haitashinikizwa na nchi za Magharibi kwa ajili ya kubadilisha sheria zake zinazowafanya watakaokutwa na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja kufungwa jela maisha.
Sheria hiyo iliyosainiwa mwezi February inaruhusu kifungo cha maisha kwa watakaokutwa na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja na kufanya kuwa uhalifu vitendo vyote vinavyohusiana na mapenzi ya jinsia moja