Mwanamuziki Hafsa Kazinja. “Niliumwa sana hadi ikaonekana nimerukwa na akili, maruhani ndiyo yaliyokuwa yananisumbua. Kuna kipindi yalikuwa yakiniambia nisile samaki wala dagaa, mara yakaniambia natakiwa kuwa mganga. “Njia zote ziligonga mwamba, nikaambiwa nisali na nimuachie Mungu, nikawa nikisali sauti zinanijia nimtukane Mungu tena matusi makubwa, nimeenda hadi kwa waganga, mashehe na walokole wakaniombea na nikapoteza pesa nyingi hadi nikauza nyumba yangu na magari lakini wapi. Nimekwenda Kanisa la Zoe ndiyo nimepona, namshukuru Mungu.
“Sasa nimeamua kuwa Mkristo, yaani nimebadili dini kwa kumaanisha, nampenda Mungu katika roho na kweli. Sijabatizwa hivyo bado sijabadili jina ila nasali Kanisa la Zoe lililopo Segerea jijini Dar