TAARIFA YA KUKANUSHA
Kumeendelea kujitokeza vikundi mbalimbali vinavyojinasibisha na Mh Edward Lowassa, miongoni mwao ni kile kinachojiita Muungano wa Marafiki wa Mh Edward Lowassa Wasio na Mipaka(MELOWAMI).
Muungano huu umetoa taarifa katika mitandao ya kijamii ukiishutumu kamati ya maadili ya CCM kuwa inamfanyia hujuma Mh Lowassa. Kwa mara nyingine tena ofisi ya Mh Lowassa inakanusha kuhusika kwa namna yoyote ile na taarifa za kikundi hicho na vingine vitakavyotoa.
Imetolewa na ofisi na Mh lowassa(mbunge)
EDWARD LOWASSA
MP FOR MONDULI CONSTITUTUENCY.
FORMER PRIME MINISTER OF THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA