Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

TAARIFA MAALUM YA POLISI JUU YA KIFO CHA SISTA NA MAJAMBAZI BONGO!!

$
0
0



30kova
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar esa salaam imetangaza msako mkali wa kuwatafuta na kisha kuwakamata walio husika katika tukio la kuua kwa kumpiga risasi kwa mtawa wa kanisa katoliki Sista Cresencia Kapuri mwenye umri wa miaka 50.

18kova
Sista huyo ambaye alikua mhasibu wa parokia ya kanisa katoriki Makoka aliiuwawa kwa kupigwa risasi June 23 eneo la Ubungo Kibangu.
Kamnda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amesema>>’Awali marehemu alikuwa ameongozana na wenzake ambao ni Sista Brigita Mbanga mwenye miaka 32,mkazi wa makoka pamoja na dereva wao Mack Patrick mwarabu’
40kova
‘Ambaye ndiye aliyekua akiendesha gari hiyo aina ya T/Hillux Pickup namba za usajili T 213 CJZ ambapo walikua wakitokea Benk ya CRDB tawi la Mlimani City,walipofika eneo la Ubungo Kibangu ili kulipa deni la chakula katika duka la Bwana Thomas Francis’
‘Ndipo walipotokea majambazi wawili wakiwa na pikipiki ambayo haikusomeka namba za usajili na mmoja akiwa na bunduki aina ya SMG wakampiga risasi ya kidole gumba cha mkono wa kulia dereva wa gani hiyo kisha kumpiga mtawa huyo risasi ya kifuani na kupora mkoba uliokuwa na pesa kiasi cha shilingi 20,000, 000 (Milioni Ishirini) na nyaraka mbalimbali za ofisi’.
 
credit: millard ayo

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>