Bibi mmoja Mkazi wa mtaa wa Nyahanga, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Rebeka Sengasenga (82), ameuawa kwa kukatwa na Shoka kichwani kwa kile kinachohisiwa kuwa ni imani za Kishirikina.
Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo limetokea leo majira ya saa tatu asubuhi katika Mtaa wa Nyahanga, wilayani humo, ambapo Marehemu Rebeka alienda nyumbani kwa mtoto wake Bundala Sengasenga alikokuwa ameitwa na mke wa Bundala kusaidia kuanika Dengu.
Muonekano wa Mwili wa Marehemu kwa nje |
Imeelezwa kuwa Merehemu Rebeka ambaye alikuwa akiishi kwa mwanae mkubwa Stanley Sengasenga katika mtaa huo alifika kwa Bundala muda huo baada ya kuitwa na Magreth Richard ambaye ni mke wa Bundala kwa ajili ya shughuli hiyo.PICHA ZAIDI>>>>>>>