kipele kidogo miaka zaidi ya 10 iliyopita lakini kadiri siku zilivyokuwa zikienda ndipo uvimbe huo ulizidi kuongezeka na kufikia usawa wa mbavu.
Akizungumza na waandishiw ahabari ambao walimtembelea nyumbani kwao alisema kuwa uvimbe huo una ambatana na maumivu makali pamoja na homa kali hasa nyakati za usiku.
Niko kwenye wakati mgumu kama mnavyoniona napata shida naomba nisaidiwe kwani nimekwenda hospitali toka kipindi hicho lakini sikupata matibabu zaidi ya kupewa vidonge tu ambavyo hupunguza maumivu lakini uvimbe uko pale pale,” alisema Nata.
Nata ambaye ana mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka (2) alisema kuwa wakati tatizo hilo linaanza alikwenda hospitali mbalimbali lakini hakuweza kupatiwa matibabu sahihi na kupelekea uvimbe huo kuongezeka hadi hapo ulipofikia na kumkosesha raha.
Somaz aidi>>>>>>>>