Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

LULU KATIKA BIFU JIPYA NA WASANII HAWA WA HIPHOP! SOMA FULL STORY HAPA

$
0
0



Baada ya msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael kuwakana waimbaji wa muziki wa kizazi kipya wanaounda kundi lijulikanalo kwa jina la mapacha kuwakana kufanyanao wimbo unaojulikana kwa jina la ‘Time For The Money’. mapya yaibuka.. 


Akizungumzia hali hiyo Kulwa wa Mapacha amesema kitendo alichokifanya Lulu ni dharau kubwa kwao na kwamba inawezekana ameona hataki kusikika kwenye wimbo waliofanya wao. 

“Sisi tuliamua kumtaja kwa respect kwa kuwa tulipenda alichofanya kwenye huo mdundo ambao sisi tuliamua kuiimbia kwa kutumia chorus yake. Lakini yeye ameamua kutu-disrespect. Sasa sisi tumeamua hata kama wimbo huo ukipata tuzo basi yeye hatutamtaja...ametudharau.”Alisema Kulwa. 

Aliongeza kuwa hivi sasa wameamua kulifuta jina la Lulu na kwamba hata wimbo huo utakapokuwa unapigwa asitajwe kabisa. 

“Sasa hivi tunasimama kama Magenge peke yetu. Tumeachana na masuala ya Lulu, hatutamtaja na tunafuta jina lake kabisa sasa hivi tunabaki Magenge tu.” 

Alipoulizwa kwa nini hawakuwasiliana naye kabla ya kuuachia wimbo huo, alijibu kuwa Alisema wao hawajawahi kuonana nae wala kuwasiliana nae hata siku moja. 

“Tungewasiliana nae vipi, si unajua hawa watoto unaweza kuwapigia simu wakaacha hata kupokea..si unajua mwanangu. Sisi tungempata wapi sasa. Tud yeye alituambia ni Lulu na sauti yake kweli ni yeye. Sasa kama anakataa bana tunaachana nae." 

Baada ya Mapacha kutambulisha wimbo wao na taarifa kumfikia Lulu leo, aliandika kwenye Instagram kwa mshangao mkubwa. 

“Mwe mwe mwe...!Mbona mnaninyasanyasa...'in Senga's voice' I swear sina idea na Huku kushirikishwa....au kuna Elizabeth Michael'Lulu' mwingine!???? Dah...hebu mliosikia hyo nyimbo labda mniambieMana nashirikishwa ki miujiza jmn.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>