Dokta Herman akitahayali baada ya tukio hilo.
Dokta mmoja aliyefahamika kwa jina la Herman amenaswa katika dispensari moja iliyopo Buguruni Kwamnyamani jijini Dar akijiandaa kumtoa mimba mwanafunzi.
Awali, kikosi kazi cha kufichua maovu cha Global Publishers (OFM), kilipewa malalamiko juu ya dispensari hiyo kuwa ni kinara wa mchezo huo mchafu wa kuwatoa mimba mabinti wadogo hususan wanafunzi wa shule za msingi.
Siku aliyonaswa, ilikuwa majira ya jioni ambapo kaka wa mwanafunzi (jina tunalihifadhi) aliandaa mtego wa kumnasa daktari huyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa rafiki wa mdogo wake kuhusu mchezo huo mchafu anaoufanya daktari huyo.
Kaka huyo aliwapigia simu makamanda wa OFM ambapo walitia timu sambamba na polisi kwenda kuweka ‘kambi’ katika dispensari hiyo kuhakikisha tukio zima linakuwa ‘recorded’.
Kaka huyo alitanguliwa katika dispensari hiyo na kubana sehemu kumsubiri mdogo wake huyo afike ‘kutoa mimba’ huku makamanda wa OFM wakiwa wameseti mitambo yao maalum katika kila engo ya eneo hilo.ANGALIA PICHA ZAIDI>>>>>>>>