MWANADADA kutoka kiwanda cha Filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amewabwatukia wasanii wenzake wanaomshutumu kwamba anatumia ndumba na kuwataka waache maneno hayo.
Nisha aliyasema hayo kufuatia hivi karibuni kuzagaa kwa tetesi kuwa alizomewa na wasanii wenzake wakimwita mchawi kutokana na mafanikio aliyoyapata kwa haraka kwenye sanaa, tofauti na wasanii wengine wanaosota kwa muda mrefu mpaka kupata mafanikio.
“Unajua siku zote mti wenye matunda ndiyo huwa unapigwa mawe, kipindi nikiwa bado sijaweza kucheza filamu zangu, yaani nikiwa chipukizi hakuna aliyekuwa ananizungumzia lakini sasa hivi wananiongelea kila kona, anayesema mimi ni mchawi basi huwa tunawanga pamoja, mimi namwamini Mungu sijui na siamini katika uchawi, mafanikio yangu ni Mungu tu na kujituma kwa bidii,” alisema Nisha.
GPL