Binti anayedaiwa kubakwa na baba yake, kupewa ujauzito na kuambukizwa Ukimwi. Picha na Florence Focus.“Amini usiamini hizi ni zama za mwisho mwanangu, mimi hili suala bado haliniingii akilini kabisa, kwani nilizoea kusikia kama hadithi kuwa mzazi ana uhusiano wa mapenzi na mwanawe, lakini leo hii yamenikuta ya kunikuta,” haya ni maneno ya Bhoke Mwita (siyo jina halisi), mama mzazi wa binti anayedaiwa kubakwa na baba yake mzazi kwa miaka minne.Bhoke anasema kibaya zaidi mwanaye amefanyiwa unyama huo na baba yake mzazi, huku akimwachia doa ambalo haliwezi kufutika milele ambao ni ugonjwa wa Ukimwi.Tukio hilo linamsababisha Wanjara kunyamaza kwanza kabla ya mahojiano, baadaye anadai binti yake kapewa ujauzito na maambukizi ya Ukimwi na baba yake, ingawa alikuwa hajitambua kuwa ni mgonjwa hatua ambayo imemuumiza na kumtia aibu kwenye jamii.
Mkazi huyo wa Mtaa wa Kigera Kibini, Kata ya Kigera, Manispaa ya Musoma mkoani Mara, anasimlia historia ya maisha yake hadi kuzaa mtoto huyo wa mwisho nje ya ndoa baada ya mumewe kufariki, lakini hatima imekuwa kugeuzwa mke mwenza.
Mwita anasita kuendelea na simlizi kabla binti yake aliyefanyiwa unyama na baba yake, hajasimulia masaibu yake: “Matatizo niliyonayo ni mengi, Mungu pekee ndiye anayefahamu, bado naongezewa msalaba mzito kama huu.”endelea>>>>>>>>>>>