Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

WAPIGANA MAKABURINI, MWILI WARUDISHWA HOSPITALI, KABURI LAFUKIWA

$
0
0

zimejikuta zikiingia katika uhasama mkubwa, kiasi cha kupigana fimbo na ngumi makaburini katika ugomvi wa kugombea kuzika mwili wa mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

Sababu kubwa ya mpasuko huo imeelezwa kuwa ni mahari, kwani wazazi upande wa mama wa mtoto huyo walikuja juu na kumzuia baba wa mtoto, Joseph Bacho mkazi wa Mtaa wa Kawajense- Madukani mjini Mpanda asishiriki katika shughuli zozote za maziko ya mtoto wake wakidai hawamtambui kwa kuwa hajatoa mahari kwa binti yao.

Inaelezwa kuwa, Joseph na mzazi mwenzake, Anna Kizo ambaye pia ni mkazi wa Mtaa wa Kawajense –Madukani walimzaa mtoto Junior Bacho nje ya ndoa ambapo hadi umauti unamfika mtoto huyo, baba yake mzazi alikuwa hajajitambulisha kwa upande wa mwanamke wala kutoa mahari.
Na kwamba, tangu kuzaliwa kwa mtoto huyo, alikuwa akiishi na kulelewa na mama yake mzazi, Anna nyumbani kwa wazazi wake katika Mtaa wa Kawajense.
Kwa mujibu wa waombolezaji ambao hata hivyo hawakuwa tayari kutajwa majina gazetini, vurugu hizo ziliibuka baada ya upande wa ndugu wa baba wa mtoto kuweka msiba nyumbani kwao na kuandaa taratibu za kumzika mtoto huyo.
Hata hivyo, kitendo hicho kilipingwa na upande wa mama wa mtoto, ukisema ndio wenye haki ya kumzika mtoto huyo ambaye hawakuwahi kumtambua kisheria baba yake mzazi.
Ndugu wa upande wa baba ulifanikiwa kuchimba kaburi, kuutoa mwili mochari na kuufikisha nyumbani tayari kwa maziko, lakini vurugu za upande wa pili ikiwa pamoja na ndugu upande wa mama kufukia kaburi, zilisimamisha shughuli zote, huku malumbano yakishika hatamu hadi askari wa jeshi la polisi kupitia kikosi chake cha kuzuia fujo (FFU) kilipolazimika kuingilia kati na kusimamia shughuli za kuurudisha mwili katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda.
Inaelezwa kitendo cha upande wa mama wa mtoto kufukia kaburi ndiko kulikochangia kuchochea vurugu hadi FFU walipoingia kati.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutokea kwa mkasa huo kwamba hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa katika vuta nikuvute hiyo pia hakuna ayekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambalo ni la kijamii zaidi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>