Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

EMMY SIZYA: WASANII WA KIKE WANANYIMWA NAFASI YA KUMILIKI FILAMU

$
0
0
 
 TANGU ilipoanza tasnia ya filamu nchini katika miaka ya 2000, unaweza kujiuliza kwa nini hadi leo wanaomiliki filamu zao wengi ni wasanii wa kiume.
Ingawa katika kuigiza filamu hizo, wanawake pia wanahusika kwa kiasi kikubwa na kufanya filamu kupendeza na kuvutia, lakini katika kumiliki ni wachache wanaozimiliki ingawa wameanza pamoja. Wasanii wengi wa kike wanasema miongoni mwa sababu kubwa za kutomiliki filamu zao, kunatokana na utumwa wa kingono wanaolazimishwa na wasambazaji, wadau na wasanii wenzao.
Wengine wakidai kwamba uhaba wa fedha, ubabe kwa baadhi ya dairekta na mpigapicha kunawafanya washindwe kufikia malengo yao. Miongoni mwa wasanii ambao wamepata suluba kutoka kwa mpigapicha, ni mwigizaji Emmy Sizya wakati anatengeneza filamu yake ya kwanza ya Tumaini langu. Anasema filamu hiyo iliyoandikwa na rafiki yake, David pia ni msanii aliyeshiriki kuigiza filamu hiyo.

 Kabla sijaanza kuigiza, rafiki yangu aliniambia, kutengeneza filamu kuna changamoto nyingi. Hasa kwa mtoto wa kike ndo balaa
anasema Sizya.
Anasema alikubaliana kupokea changamoto zote zitakazojitokeza, ndipo akaanza maandalizi ya filamu hiyo mwaka 2012 huku akimteua Kulwa Kikubwa kama mwongozaji wa filamu hiyo.
 Nilianza filamu nikiwa na mtaji wa kutosha kuweza kukamilisha mapema na kuweza kuingiza sokoni
alisema na kuongeza kuwa hakupata tabu katika kuhakikisha anapata wasanii kwa ajili ya filamu yake, kuwalipa kulingana na kazi waliyokuwa wakiifanya.
Anasema tatizo likaja baada ya kukamilika filamu hiyo, ndipo usumbufu ulipoanza kuchomoza. Filamu iliisha mapema kama ambavyo alifikiria, lakini anasema baada ya kukamilika, ndipo mpigapicha aliposafiri bila ya kukamilisha kazi hiyo. Anasema ni kawaida sana wapigapicha wa filamu za Tanzania kuchukua kazi zaidi ya moja, mbabe ndiye anaweza kupewa kazi yake haraka hata kama atakuwa wa mwisho.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>