Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

EXCLUSIVE PART 2 YA NINI KILIMUUA MWANAMUZIKI MAARUFU WA VIJANA JAZZ CHIRIKU HEMEDI MANETI? MSIKIE MBEBZ WAKE LIVE!!

$
0
0


                                                                Kida Waziri



Imeandikwa na  MOHAMMED KUYUNGA
MWANAMUZIKI wa zamani wa Bendi ya Vijana Jazz ‘Pambamoto’ Kida Waziri anaendelea kusimulia kile kilichompata kabla na baada ya kifo cha mzazi mwenzake, aliyekuwa kiongozi wa bendi hiyo, Hemed Maneti Ulaya.
Kida amepitia misukosuko mingi, hebu endelea kufuatilia maelezo yake ya kusisimua…
Ndugu wamchukua mfanyakazi
Majirani walimsakama na kuwaambiwa ndugu wa mfanyakazi wake wa ndani kwamba watampoteza ndugu yao kwa kuwa familia hiyo imeathirika na Ugonjwa wa Ukimwi, ndipo  ndugu wa mfanyakazi huyo walipofika kwake na kumwambia kuwa wamekuja kumchukua msichana wao ili wamrudishe kwa wazazi wake.
“Niliumia sana, kwani walidai kuwa wazazi wa mtoto huyo wanakaa mbali, wao hawataki kuingia kwenye matatizo… wakamchukua,” alisema Kida.
Mtoto wake ahamishwa shule
Kama vile haitoshi, majirani waliendelea kumsakama Kida, waliwaambukiza mpaka watoto wao kasumba ya kuinyanyapaa familia yake kwa kusema kuwa wote wameathirika kwa Ukimwi.
“Hata watoto waliokuwa wakisoma na Waziri  katika Shule ya Msingi ya  Ananasifu walikuwa wakimsakama na kumtenga kwa kumwambia kuwa ana ukimwi na waliogopa asije akawaambukiza, ilinibidi nimwamishe shule na kumleta  Shule ya Msingi Mwongozo iliyopo Kinondoni.”
Hakuweza kukopeshwa fedha
Bado baadhi ya ndugu walimfuata Kida na kumuuliza kama  alikuwa akijisikia kuumwa, au alishaanza kutokwa na  vipele sehemu yoyote ile ya mwili wake.
“Yalikuwa ni maneno makali kwangu, yaliniumiza sana Mohammed,  sikuwa na moyo wa chuma, nilikuwa nikijifungia ndani  na kuwakumbatia wanangu na kisha kulia kwa uchungu, hawa ndiiyo walikuwa faraja yangu”alisema Kida huku machozi yakimlengalenga.
Baadhi ya majirani hawakutaka hata atumie vyombo vyao vya kulia chakula na wengine walikataa kumkopesha pale alipoomba  mkopo  kwa ajili ya shida za familia yake.
“Waliniambia nani anaweza kumkopesha mfu na kudai kuwa siku zangu zilikuwa zikihesabika , ilinitesa  na kuniumiza sana, sikuwa naujua mustakabali  wa maisha yangu kwamba yatakuwaje mbele ya safari,” alisema.
Kida anasema kuwa hakuwa na mtu wa kumfariji katika kipindi hicho kigumu zaidi ya wanawe, hakupata faraja ya mawazo, mfariji na mshauri wake pekee alikuwa ni mzazi mwenziye (Maneti) ambaye alishafariki dunia.
Alichemsha mapapai
“Sikuweza kula vizuri, kwa kuwa sikuwa nikipata fedha za kutosha,  ilifikia siku moja nilichemsha mapapai na kula na wanangu… siku hiyo sitaisahau maishani mwangu..
“Mvua kubwa ilikuwa imenyesha nilikuwa nimetoka Posta (mjini) kwa miguu, usiku ulikuwa mwingi nikarudi  hadi Kinondoni bila ya kuwaogopa wahuni njiani, nilipofika njaa ilikuwa ikiniuma na wanangu hawakuwa wamekula.
“Kila kitu kilikuwa kimelowana na mvua, nikachukua novo (kitabu) cha mpangaji wangu na kuwashia moto kuchemsha mapapai, kilichonikuta  baada ya mpangaji kujua nimechana kitabu chake ilikuwa ni balaa,” anasimulia.
Wapenzi waliogopa kumtunza
 Kida anasema katika hatua zake za mwisho Vijana Jazz pamoja na kwamba hakuwa akilipwa na hata posho zake za Jumapili na alichoshwa na maneno ya kashfa.
“Hata wapenzi waliokuwa wakinitunza fedha, hawakutaka kunigusa, nilifadhaika sana kwa kuwa sikuwa najua mustakabali wa maisha yangu,” aliongeza.
Alitakiwa kurudishwa Tanga
Kuna baadhi ya ndugu walipendekeza arudishwe Tanga ili kuhofia gharama za kumsafirisha akiwa ameshafariki.
Aimbwa kwenye daku
“Kuna wale waliokuwa wakiimba nyimbo za kuwaamsha watu kwa ajili ya kula daku wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, walinitungia wimbo na kusema kuwa bwana wangu (Maneti) amekufa kwa Ukimwi na miye nina ugonjwa huo…” alisema Kida na kushindwa kuendelea.
Madaktari wanong’ona
Ilitokea wakati, Kida aliumwa chembe kutokanana kufanya mazoezi ya nguvu na  Bendi ya Vijana Jazz. Hali ilikuwa mbaya sana na watu wakaanza kusema kwamba virusi vilikuwa vimemchachimaria.
“Sikuwa na mtu wa kunisaidia  kuna dada yang aitwaye Amina aliyekuwa akifanya kazi Tancot House akaniita ili niende kuchukua sick sheet (hati ya matibabu) kwa ajili ya kwenda kutibiwa katika zahanati ya kazini kwao.
“Nilitibiwa lakini kuna kitu kilinishangaza, madaktari na manesi walinichangamkia sana, lakini kabla hata hawajanipima wakaanza kunong’onezana, moja kwa moja nilijua hisia zao kuhusu mimi, nilijua nao wanajua kuwa nimeathirika, ilinichanganya sana.
“Nilitibiwa lakini sikupata nafuu kwa haraka, kuna wakati niliamua kutoroka katika zahanati hiyo bila ya ruhusa ya mtu yeyote, nikawa natembea maneo ya mjini, hali yangu ikiwa bado haijatengemaa, ghafla mbele yanga wakatokea  Mwanamuziki Jah Kimbute na Meneja wake, Abdul Kelly wakanichangamkia sana,” alisema Kida.
Pamoja na Kimbute na Kelly ambao walikuwa ni marafiki wa karibu wa kaka yake Kida aliyekuwa akiishi Uingereza, kumchangamkia Kida lakini yeye aliendelea kulia.
“Kila walichokokuwa wakiniuliza nilikuwa ninalia, baadaye niliwaambia kwamba nilikuwa naumwa, wakakodi teski na kunipeleka katika zahanati ile ile ili niweze kupata vyeti vyangu na kujua tatizo lililokuwa likinisumbua.
“Bahati hatukuwata wale madaktari waliokuwa wakinihudumia, walikuwa wameenda kula chakula cha mchana, tuliwasubiri mpaka Kimbute na Kelly wakakata shauri kunipeleka kwa Dk. Khan.”
Maneti alitupiwa jini
Wakiwa njiani, Kimbute na Kelly walimwambia Kida kwamba asiwe na hofu, alikuwa mzima wa afya njema ila alikuwa ametupiwa jini akiwa katika  Bendi ya Vijana Jazz.
“Waliniambia  hata mzazi mwenzangu, Maneti alikuwa ametupiwa jini na kunitaka nikipona nisirudi tena katika bendi ya Vijana Jazz,  kwani nami nitakufa kama alivyokufa Maneti,” alisimulia Kida.
Baada ya kufika kwa Dk. Khan, Kida aliwekewa dripu na kupewa mapumziko na hatimaye aliweza kujisikia vizuri na kuweza kutoka hospitali.
Safari Austria
Kimbute ambaye alikuwa akimiliki Bendi ya Roots & Culture alikuwa amepata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye Tamasha la Wiesen Sunplshash nchi Austria ambalo lilishirikisha bendi 20 kutoka katika nchi mbalimbali  duniani, akamwambia Kida kwamba walikuwa wakitafuta  mwanamuziki wa kike kwa ajili ya kwenda naye kwenye tamasha hilo.
“Ilikuwa ni kama bahati yangu, sikutarajia  kama ningeweza kupata nafasi hiyo ya kwenda Austria ambayo ilikuwa ni mojawapo ya  mikakati yangu na Maneti kwenda nje ya nchi, nikaanza taratibu  za kuondoka na Kundi la Roots & Culture,”alisema.
Mwanasiasa amgomea kusafiri
Mwaka huohuo wa 1990 baadhi ya viongozi wa Vijana Jazz wakaanza harakati za kumwajiri ili aitumikie Vijana Jazz lakini kwake ilikuwa ni vigumu kuachana na safari hiyo.
“Maneno yakanza, lakini nilisimama imara na kuhakikisha kuwa natimiza azma yangu ya kuondoka na Roots & Culture kufanya tamasha nje ya nchi,” aliongeza Kida.
Mmoja wa wanasiasa ambaye kwa sasa ni mbunge (jina lake tunalihifadhi) alimfauata Kida na kumwambia kwamba asijisumbue kusafiri kwa kuwa ameathirika na Ukimwi.
“ ….( anamtaja jina) aliniumiza sana, aliniambia kuwa alikuwa na uhakijka kwamba Maneti amefariki kwa Ukimwi na yeye alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa mstari wa mbele kwenda Nairobi, (Kenya) kumchukulia vidonge vya Kemroni ambavyo vilidaiwa kuwa vilikuwa na uwezo wa kuponya Ugonjwa  wa Ukimwi lakini akafariki kabla ya zoezi hilo halijatimia,” alisema Kida.
 Apelekwa kupimwa Ukimwi
Hapa Kida alisimulia kwa masikitiko mazito na mara kwa mara aliangua kilio, ilifikia hatua mwandishi wa makala haya alilazimika kumbembeleza ili aweze  kuendelea kusimulia kilichotokea pale alipopelekwa na mwanasiasa huyo kupimwa Ukimwi katika hospitali moja binafsi, pia kulikuwa na mkakati wa kumpeleka kwa mganga mmoja maeneo ya Kariakoo, Mtaa wa Swahili na Amani, jijini Dar .
Nini kiliendelea? Usikose kufuatilia kilichotokea katika kesho.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>