Ni ajari mbaya sana lanini kama unavyoona hapo lakini kwa ubora wa mabehewa wamefariki watu wanne tu R.I.P
Mabehewa yameburuzana mpaka karibu na mto kama unavyoona na hakuna hata behewa mojalililopinda au kupasukakama inavyoonekana hapo pichani hapo mbele palikutana na miti, mawe, na visiki lakini angalia vioo havikua siraha ya kuwachinjia watu walokuemo ndani ya behewa maana havikupasuka
inaonekana hapo wakiyanyanyua mabehewa yaloanguka ili waanze kufanya uchunguzi wa ninini kilichosababisha ajali hii je ni train yenyewe au ni deleva?Kama uionavyo picha hapo juu mabehewa baada ya kusimamishwa yamenyooka kwenye reli kama vile hayakupata ajari kwa sababu hayakupinda hata kidogo hata magurudumu hayakutoka hata moja kwa sababu viwango vya utengenezaji vinafuatwa inavyotakiwa kwa ajiri ya usalama wa abiria.
Na wiki hiyo hiyo baada ya kufanya uchungusi wanasiasa waliwarazimisha wataalam wa treni waweke mtambo kwenye kila treni likiwa kwenye kona kama dereva akipitiwa kupunguza breki lijisimamishe lenyewe na wameongeza dereva wa pili ili mmoja ikitokea bahati mbaya ameumwa ghafla au amesinzia mwengine anaongoza treni yote hayo kuhakikisha haitatokea tena ajari ya aina hii, jamaa hawaamini neno la mungu kapenda wanaamini kuna uzembe aidha wa mashine au wa binaadam, na wanawapenda wananchi wao
Hii nimeileta ni kwa ajiri ya ndugu zetu wa TBS ambao mlopewa madaraka ya kuangalia viwango na ubora ya vitu tunavyovitumia kila sibu najua mabehewa hatuyatengenezi sisi hapa nchini bali mabodi ya MABASI yanatengenezwa hapa hapa nchini tusaidieni aidha muende nje mkaangalie ni nini cha kuangalia ubora wa bodi la basi si rangi na taa zikiwa nzuri basi ni zuri,, mabasi yanatuuwa sana hapa nchi na yanawaweka watu wengi kwenye ulemavu wa maisha ni hasara kubwa sana kwa taifa vijana wengi wanakosa elimu baada ya mfadhiri wa elimu yake hawezi tena kusaidia ili asome aidha ameuawa na kwenye basi ama amejeruhiwa vibaya kutokana na viwango vya utengenezaji wa mabasi haueendani, hakuna ajari ndogo hapa nchini hata ukisikia basi limegonga nyoka utasikia watu 32 wameuwawa kwenye ajari hiyo maana basi linamong'onyoka kama limetengenezwa na mabua na makaratasi: TBS mmepewa kazi tunaomba mtusaidie na ndugu zangu watanzania tujitahidi tuwaeleze wawakirishi wetu tulowachagua huko majimboni watusaidie wakiwa huko Dodoma watilie mkazo ubora wa mabasi laa sivyo yatatumaliza maana sijasikia wakizungumzia, maana haya mabasi yamegeuka kuwa viwembe vinakata shingo tu kila siku... siku njema people... LE MUTUZ