BAADA ya kuzagaa kwa taarifa mbalimbali kwamba mwigizaji wa Bongo, Kajala Masanja anachepuka nje, ameibuka na kukanusha madai hayo akisema hayana ukweli wowote.
Mitandao mbalimbali ya kijamii imekuwa ikiposti taarifa mbalimbali zinazomhusisha Kajala kutembea na wanaume tofauti kitu ambacho mwenyewe amesema hakina ukweli na wanaosambaza uvumi huo, wakome.Akizungumza na mwanahabari wetu Julai 3, mwaka huu alisema wanaoeneza habari za yeye anachepuka wanamtafuta ubaya kwani hana mpango wowote wa kuolewa wala kuishi na mwanaume kwa sasa.“Waniache, mtu akisema nina mwanaume alishawahi kuniona? Sina mwanaume mwingine zaidi ya mume wangu,” alisema KajalaKwenye mahojiano hayo, Kajala alisisitiza kuwa, haoni sababu ya yeye kuchepuka wakati mumewe Faraja Augustino yupo hai na anaamini ipo siku atatoka gerezani na ataendelea na maisha ya ndoa yake kama ilivyokuwa zamani.endelea >>>>>>>>>