Stori: Musa Mateja
MOYO unauma! Staa wa R&B Bongo, Juma Khalid ‘Jux Vuitton’ amekiri kuteswa na ishu ya mwanamitindo Jacqueline Fitzpatric Cliff ‘Jack Patrick’ akiomba asiulizwe habari za modo huyo aliyekuwa mpenzi wake ambaye kwa sasa yupo nyuma ya nondo kwa madai ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’ huko Macau, Hong Kong nchini China.
Staa wa R&B Bongo, Juma Khalid ‘Jux Vuitton’
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, jamaa huyo alisema kuwa kwa sasa hapendi kabisa kusikia mtu akimuuliza habari zinazohusiana na mpenzi wake huyo, kwani zinamtoa kwenye ‘mudi’ na badala yake ana mambo mengi ya kuzungumza.
‘Jux Vuitton’ akiwa na Jack Patrick.
“Naomba mtu asiniulize ishu za Jack, zinanitibua na zimeshazungumzwa sana hivyo sioni kipya cha kuzungumzia zaidi ya muziki wangu, kwa sasa nina projekti mpya kibao zinakuja,” alisema Jux anayetamba na ngoma ya Nitasubiri aliyomuimbia Jack.