Ingawa hayupo Tanzania lakini hakungoja mpaka arudi ndipo akabidhi zawadi hii badala yake alichokifanya ni mara baada ya kukamilisha kila kitu kinachoihusu gari hii Diamond Platnumz aliwapatia mameneja wake kwa ajili ya kuiwasilisha kwa mama yake.
Ni Toyota Lexus New Model ambapo Babu Tale amesema imegaharimi milioni 38.1 ambapo milioni 35 imetumika kulinunulia gari hilo mpaka kuingia Tanzania na Milion 3.1 imetumika kulipamba na kuweka Music System pamoja na seat Cover.
Zawadi hii ameitoa Diamond kwa mama yake kama zawadi kwa ajili ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa mama yake ambaye amesema ametimiza miaka 55, mama yake amesema hakutegemea zawadi hii na anamuombea mwanae kwa Mungu afanikiwe zaidi.
Baada ya kufuturu Meneja wa Diamond Babu Tale alitangaza utaratibu wa kuzindua kwanza video mbili za Diamond kwa watu waliokuwepo hapo kisha utaratibu mwingine ukaendelea ikiwemo kumuimbia mama yake Diamond kisha kukabidhiwa gari yake.
Hizi ni picha kuanzia wakati wa kufuturu hadi mama yake Diamond anakabidhiwa gari hiyo mbele ya mastar kadhaa akiwemo Wema Sepetu,Shettah,Madee,Profesa Jay,Aunt Ezekiel na wengine kibao.
M