LEO July 11 ndo siku ambayo usaili wa kuwatafuta washiriki watakaoiwakilisha Tanzania katika reality show ya Big Brother nchini Afrika Kusini utaanza kufanyika.
Mara nyingi zinapokaribia siku za usaili mashabiki mbalimbali huweka ubashiri wao wa mastaa ambao wanadhani wanafaa kwenda kutuwakilisha.
Vanessa Mdee ni miongoni mwa mastaa mabao walitajwa na baadhi ya watu kuwa anaweza kufaa kama atawania nafasi hiyo mwaka huu.
Hiki ndicho alichojibu Vanessa kama yuko tayari kuwaridhisha mashabiki wanaotamani achukue fomu na kushiriki kwenye usaili wa kupata nafasi hiyo.
will be so defeated yaani ntatoka siku ya tatu afu ntawa disappoint wale waliokuwa wanapenda niwe pale”.
Licha ya yeye kutokuwa na wazo la kushiriki ila amemtaja mtu anayedhani anaweza kufaa kwa nafasi hiyo.
Raheem Da Prince wa Times FM
“I think Rahim should Try, Rahim da Prince. Rahim I think he understands a lot about the world halafu pia ana personality he is very outgoing so nadhani angeweza kufanya vizuri pale”.
Lakini pia amemtaja mtu ambaye hastahili na asiyetakiwa hata kujaribu kuchukua fomu:
“Nadhani mpoki asiende”.LOL!
Usaili wa kuwatafuta wawakilishi wa Tanzania kwenye Big Brother utafanyika kwa siku mbili kuanzia leo July 11 na July 12 katika hotel ya New Afrika jijini Dar.